MSHAMBULIAJI
hatari wa Simba, Mrundi Amisi Tambwe amesema timu yao imekuwa na wakati
mgumu katika mechi za mikoani kutokana na wapinzani wao kucheza kwa
kuwakamia.
Simba ilipoteza mchezo wake wa kwanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kukubali kipigo kisichotarajiwa cha bao1-0 dhidi ya ‘maafande’ wa Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga juzi.
kikosi cha Simba kikiwa safarini kurejea jijini Dar es Salaam leo mchana, Tambwe amesema kuwa mechi ya juzi ilikuwa ngumu sana kwa timu yao kwa vile Mgambo walicheza mpira wa mabavu.
“Ilikuwa mechi ngumu sana kwa sababu Simba inakamiwa sana mikoani. Tulipigwa sana kiatu jana, wapinzani wetu walicheza kwa nguvu nyingi badala ya akili. Tutaendelea kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi yetu inayofuata dhidi ya Mbeya City,” amesema Tambwe.
“Kulikuwa na matukio ya kishirikina kabla ya mchezo lakini siamini mambo hayo. Kikubwa ni kufanya kazi kwa kujituma badala ya kuendekeza mabo ambayo hayana maana,” amesema zaidi Tambwe.
Siku moja kabla ya mchezo huo kupigwa, uongozi wa Uwanja wa Mkwakwani ulikaririwa ukidai kuwa uliokota mayai ya ‘Kiarabu’ yaliyokuwa yamewekwa uwanjani kwa imani za kishirikina.
Kwa ushindi huo, Mgambo wamelipa kisasi cha kufungwa mabao 6-0 katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Uwanjja wa Taifa jijini Dar es Salaam Septemba 18 mwaka jana na wamepanga hadi nafasi ya 10 ya msimamo wa ligi wakiwa na pointi 13 walizokusanya katika mechi 17.