Social Icons

Pages

Wednesday, 12 February 2014

SCOLARI ATEUA KIKOSI CHA BRAZIL KUIVAA BAFANA BAFANA!


BRAZIL_SOCCER_FANSKOCHA wa Brazil Luiz Felipe Scolari ameteua Kikosi chake ambacho Machi 5 kitacheza Mechi ya Kirafiki na Afrika Kusini na wapo Wachezaji wawili wapya pamoja na Kipa wao Nambari Wani, Julio Cesar, licha ya kutocheza Mechi Klabuni kwake Msimu wote huu.JULIO_CESAR
Wachezaji walioteuliwa ni wale wanaocheza Ulaya na Scolari amesema ataongeza Wachezaji watatu wanaocheza Klabu za Nchini Brazil.
Brazil inatarajiwa kutangaza Kikosi chao kitakachocheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Nchini kwao hapo Mei 7 na wao watacheza Mechi ya Ufunguzi ya Fainali hizo hapo Juni 12 dhidi ya Croatia.
Baada ya Mechi na South Africa, Brazil itacheza Mechi mbili za Kirafiki kati ya Juni 3 na 6.
Kuhusu Kipa Cesar, ambae hajacheza Mechi akiwa na Klabu yake QPR ya England, Scolari amesema anategemea Kipa huyo kupata Mechi nyingi na Klabu yake mpya inayocheza MLS huko Marekani, Toronto, ambayo Wiki iliyopita amehamia kwa Mkopo.
Wachezaji wapya ambao wamo kwenye Kikosi cha Brazil ni Beki wa Bayern Munich, Rafinha, na Kiungo wa Manchester City, Fernandinho.
Chelsea imetoa Wachezaji watatu ambao ni Oscar, Ramires na Willian.
KIKOSI CHA BRAZIL:
KIPA: Julio Cesar (QPR/ENG)
MABEKI: Thiago Silva (Paris SG/FRA), David Luiz (Chelsea/ENG), Dante (Bayern Munich/GER), Dani Alves (FC Barcelona/ESP), Rafinha (Bayern Munich/GER), Marcelo (Real Madrid/ESP)
VIUNGO: Paulinho (Tottenham/ENG), Fernandinho (Manchester City/ENG), Luiz Gustavo (Wolfsburg/GER), Ramires (Chelsea/ENG), Oscar (Chelsea/ENG), Willian (Chelsea/ENG)
MASTRAIKA: Neymar (Barcelona/ESP), Hulk (Zenit St Petersburg/RUS), Bernard (Shakhtar Donetsk/UKR).
 
FULU VIWANJA