TIMU
ya Atletico Madrid jana ilikula ngwala katika mbio zake za ubingwa wa
La Liga baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Osasuna, hivyo kuwaacha Real
Madrid wajinafasi kileleni kwa pointi tatu zaidi.
Mabingwa
Barcelona na vinara Real walilazimishwa sare kwenye Uwanja wa Osasuna,
El Sadar mjini Pamplona mapema msimu huu na Atletico ikadondoka jana.
Alvaro Cejudo alifunga bao la kwanza dakika ya sita wakati makosa ya beki wa pembeni, Juanfran
yalimruhusu Emiliano Armenteros kufunga bao la pili dakika ya 21 kabla
ya Roberto Torres kufunga la tatu dakika ya 42. Atletico inabaki na
pointi 60 sawa na Barcelona iliyo katika nafasi ya pili kwa wastani
mzuri wa mabao, wakati Real pointi 63 juu yao.
Majanga: Diego Costa na David Villa wakijiandaa kuanza mpira baada ya kufungwa moja ya mabao matatu ya jana na Osasuna

Tumemaliza kazi: Roberto Torres akishangilia baada ya kufunga bao la tatu jana