Social Icons

Pages

Thursday, 27 February 2014

AL AHLY WAFANYA MAZOEZI UFICHONI



Mabingwa wa Afrika, Al Ahly wameendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam huku kila kitu kikifanyika kwa uficho.


Tayari Ahly wamefanya mazoez mara mbili jijini Upanga na wamekuwa hawaruhusu mtu yoyote kuingia na kushuhudia mazoezi yao kwenye Sekondari ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) ya Upanga jijini Dar.

Kawaida Ahly imekuwa moja ya timu makini sana wanapofikia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na muda mwingi wamekuwa na hofu ya kuhujumiwa.

Mechi yao dhidi ya Yanga itakuwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar na inatarajiwa kuweka rekodi ya watu kwa kuwa wamepania kuwaona Waarabu hao wakishindwa kwa kuwa Yanga haijawahi kuwafunga tokea mwaka 1982
 
FULU VIWANJA