MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yusuph
Manji, aliibua cheleko ndani ya Mkutano wa klabu hiyo, baada ya kumtaka
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo Ibrahim Akilimali kuacha
kuzungumza ovyo ovyo katika vyombo vya habari wakati Katiba ya klabu yao
haimpi mamlaka.
Manji aliyasema hayo, katika Mkutano wa mwaka wa chama hicho uliofanyika
katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, baada ya kujibu
swali la mwanachama Msham Wazir ambaye ni Mwenyekiti wa Tawi la Bunju
lilohoji kuwa, Wanachama hawatambui nani ni nanni ndani ya klabu kwa
kuwa kila mtu anajifanya msemaji huku akimtolea mfano Akilimali.
Baada ya swali hilo, wanachama
waliofurika katika ukumbi huo, walisimama na kushangilia na kumfanya Makamu
Mwenyekiti Clement Sanga aliyekuwa akiongoza Mkutano huo kukabidhi rungu hilo
kwa Manji baada ya yeye kutoa ufafanuzi kuwa, Katiba ya Yanga hakuna kifungu
kinachowapa mamlaka wazee kuzungumza.
“Katiba ya Yanga haiwatambui wazee
kabisa, na mtu akinielewa vibaya sawa tu, kwani hakuna sehemu ya katiba
inazungumzia wazee, kwani Msemaji Mkuu katika klabu ya Yanga ni Mwenyekiti,
Ofisa habari na hata mimi nazungumza endapo Mwenyekiti akiwa hayupo au
ameniagiza,”alisema Sanga.
Aidha baada ya Sanga kujibu hivyo,
alimkabidhi Manji jukumu la kufafanua suala hilo na kusema kuwa, Akilimali ni
Mzee wake lakini anakuwa mvunjifu wa katiba ya Yanga kwa kusema sema katika
vyombo vya habari mambo ambayo hayastaili kuzungumzwa.
“Akilimali anaongea kupita kiasi katika
vyombo vya habari, kwani wewe sio msemaji wa klabu jamani, unavunja katiba ya
Yanga, mambo ya nyumbani unaongea tu, eti Kaseja kafanyaje, jamani acha kufanya
hivyo,”alisema Manji huku akiwaomba ridhaa wanachama waamue nini cha kumfanya
Akilimali na kuwafanya wanachama kushangilia mwanzo mwisho.
Baada ya kusema hayo, Manji alinyanyuka
katika kiti alichokuwa amekaa na kumfuata Akilimali na kuanza kuzungumza naye,
huku wanachama wakishangilia na wengine kuzomea kitendo hicho.
Akizungumzia sakata hilo, Akilimali
alikiri kukiuka katiba ya Yanga, na kusema kuwa, anahisi alipandwa na wazimu
bila kujijua na ndio sababu ya kuongea katika vyombo vya habari bila idhini ya
uongozi wake.
“Mimi kusema kweli sina kinyongo
kabisa, na uongozi wangu, wamenizuia nisiongee katika vyombo vya habari, basi
nitafanya hivyo, naisi ni wazimu tu na ushabiki ulinipanda, nawaheshimu na
kuwasikiliza viongozi wangu, kama wamenipa onyo sawa tu,”alisema