NYOTA wa Bayern Munich, Franck Ribery ameuponda mfumo wa upigaji kura za kuchagua Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, Ballon d'Or na kusema alistahili zaidi kushinda tuzo hiyo kuliko Cristiano Ronaldo, kwa sababu alishinda mataji matano mwaka 2013, wakati mpinzani wake wa Real Madrid hakushinda chochote.
Mfaransa huyo alikubali kushika nafasi ya tatu nyuma ya mshindi, Ronaldo na Lionel Messi aliyekuwa wa pili katika sherehe za tuzo zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi Jumatatu iliyopita na pia amesema tuzo binafsi si muhimu kwake.


