UMAARUFU
wa Jose Mourinho na mafaniko aliyoyapata kutwaa mataji matatu ya Ligi
Kuu ya Mabingwa Ulaya, vimetokana na mfumo wa uchezaji wa timu
anazofundisha, kucheza kwa kujihami zaidi, maarufu kama kupaki basi.
Lakini
huwezi kuamini leo Mourinho anaulaani vikali mfumo huo wa uchezaji,
akiuita wa karne ya 19, ingawa yeye ameutumia miaka ya karibuni tu karne
hii na kumjengea heshima na umaarufu mkubwa.
Baada
ya kulazimishwa sare ya 0-0 jana na West Ham United katika mchezo wa
Ligi Kuu ya England, kocha huyo wa Chelsea amemkandia kocha wa wapinzani
wake, Sam Allardyce kucheza soka ya karne ya 19.
Usiku wa jana The Hammers ilipiga shuti moja tu langoni mwa Chelsea iliyopiga mashuti 39 kwenye lango la wapinzani wao hao.
“Hiyo
si ligi bora katika dunia ya soka, hii ni soka ya karne ya 19. Mbaya
mno. Ninamaanisha nini kusema soka ya karne ya 19? Inasababisha
kuumizana.
“Kudanganya,
lakini sijui kama hiyo ni kauli nzuri. Kipa alipoteza muda, si baada ya
dakika 70, bali kuanzia dakika ya kwanza. Mabeki kumi kwenye boksi.
Ngome ngumu.
“Ni vigumu kucheza mechi ya soka ambayo timu moja tu inataka kucheza. Nilimuambia Big Sam (Allardyce).
“Wanataka
pointi, lakini kwa sababu wanataka pointi, kuja hapa na kutocheza na
kufanya kama walivyofanya… inakubalika? Labda ndiyo. Siwezi kuwa
mlalamishi sana, kwa sababu kama ningekuwa kwenye mazingira yao,
sifahamu, ningefanya kama wao? Labda ningefanya,” alisema Mourinho.

Hasira: Kocha wa Chelsea alikasirishwa na mfumo wa uchezaji wa kujihami wa West Ham usiku wa jana

