
Kwa Miaka miwili iliyopita, Azam FC wamekuwa Mabingwa wa Mapinduzi Cup.
Katika Mechi ya kwanza hii leo Azam FC
waliongoza 2-0, kwa Bao za Chipukizi wao Joseph Kimwaga, lakini KCC
wakazinduka na kuichapa Bao 3-2.
Baada ya Mechi hiyo, Simba walitinga
Amaan Stadium na kubanwa na URA hadi Mapumziko kwa Bao kuwa 0-0 lakini
Kipindi cha Pili Bao za Joseph Owino na Amri Kiemba ziliwapeleka
Fainali.
Simba watacheza Fainali Jumatatu na KCC ambayo walikuwa nayo Kundi B kwenye Mashindano haya na kutoka 0-0 katika Mechi yao.
RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI
Jumatano Januari 8
Gombani Stadium, Pemba
KMKM 0 URA 1
Azam FC 2 Clove Stars 0
Amaan Stadium
Tusker 0 KCC 0 [KCC imesonga kwa Penati 4-3]
Simba 2 Chuoni 0
NUSU FAINALI
Ijumaa Januari 10
SAA 10 JIONI: Azam FC 2 KCC 3
SAA 2 USIKU: URA 0 Simba 2
FAINALI
Jumatatu Januari 13
Amaan Stadium
SAA 10 JIONI: Simba v KCC