Social Icons

Pages

Monday, 23 December 2013

TRESOR MPUTU AIHAMA RASMI TP MAZEMBE

STAA wa TP Mazembe Tresor Mputu ameihama Klabu hiyo ya Lubumbashi, Nchini Congo DR na kuhamia Klabu ya Kabuscorp, ambao ni Mabingwa wa Angola, na kusaini Mkataba wa Mwaka mmoja wenye thamani ya Euro Milioni 2.
Mputu, mwenye Miaka 28 na ni Mchezaji wa Kimataifa wa Congo DR, atakuwa akilipwa Euro 40,000 kwa Mwezi.
Ingawa Mashabiki wa TP Mazembe walikuwa hawataki Staa huyo aondoke, Klabu hiyo imetoa Taarifa kuwapoza Mashabiki hao kuwahakikishia Klabu haitayumba kwa kuondoka kwake.
TP Mazembe inao Wachezaji wawili wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Mputu amekuwa na TP Mazembe kwa zaidi ya Miaka 10 na kuisaidia kutwaa Ubingwa wa Afrika Mwaka 2009 na 2010 na pia kuifikisha Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu Mwaka 2010 huko Abu Dhabi, Falme za Nchi za Kiarabu ambako walifungwa Bao 3-0 na Inter Milan waliotwaa Ubingwa wa Dunia.
Januari 2012, Kabuscorp iliushangaza Ulimwengu baada ya kumsaini Gwiji wa Brazil, Rivaldo, ambae alidumu Msimu mmoja tu.
 
FULU VIWANJA