
Tottenham Hotspur imempa Ofa Tim Sherwood kuwa Meneja wa muda hadi mwishoni mwa Msimu.
Ofa hiyo imetoka baada ya Mkutano wa
kutwa nzima kati ya Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy, na Tim
Sherwood uliofanyika kwenye Kituo cha Mazoezi cha Enfield ambacho ndio
cha Klabu hiyo.
Sherwood, ambae amekuwa akiiongoza Spurs
kwa Mechi mbili baada ya kutimuliwa Andre Villas-Boas Wiki iliyopita,
alikuwa akifanya kazi kama Mratibu wa Ufundi Klabuni hapo pamoja na
kuzifundisha Timu za Rizevu na Vijana.
Katika Mechi yake ya kwanza Jumatano
iliyopita, Sherwood aliiongoza Spurs iliyofungwa 2-1 na West Ham na
kubwagwa nje ya Capital One Cup na Jumapili walicheza Mechi ya Ligi Kuu
England huko St Mary na kuichapa Southampton Bao 3-2.
Uteuzi huu kwa Sherwood, mwenye Miaka 44
na ambae alizichezea Spurs na Blackburn Rovers, ni kinyume na matakwa
yake binafsi ambapo mara baada ya Mechi na Southampton alitamka hataki
kazi ya muda.
Inaaminika Tottenham wanataka Meneja mzoefu lakini walengwa wao wote hawawezi kupatikana hivi sasa hadi mwishoni mwa Msimu.
Mmoja wa hao ni Mholanzi Louis by Van
Gaal, mwenye Miaka 62, ambae aliwahi kuwa na Barcelona, Ajax na Bayern
Munich, na sasa ana Mkataba wa kuifundisha Timu ya Taifa ya Holland hadi
mwisho wa Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani.