DA
BI ya LONDON ilichezwa Emirates huku
Jiji la London likikumbwa na Mvua kubwa na upepo mkali na Bigi Mechi hii
iliyongojewa kwa hamu kati ya Arsenal na Chelsea kumalizika 0-0.
Matokeo haya yameibakisha Liverpool
ikiwa bado kileleni wakifungana Pointi na Arsenal, wote wakiwa na 36, na
Man City wakishishika Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma huku Chelsea,
waliofungana kwa Pointi na Everton, wakiwa Nafasi ya 4.
Ukiondoa shuti la Frank Lampard kupiga
Posti Kipindi cha Kwanza hakuna Nafasi za wazi kabisa zilizotokea katika
Mechi hii na iliwachukua Arsenal hadi Dakika ya 85 kupiga moja ya
Mashuti yao mawili tu yaliyolenga Goli katika Mechi nzima.