HII
ni Dabi ya Jiji London ambayo leo inazikutanisha Uwanjani Emirates,
Arsenal na Chelsea, huku Arsena
l ikiwania ushindi kurudi tena kileleni
mwa Ligi Kuu England ambako Jumamosi ilienguliwa na Liverpool lakini
Arsenal, chini ya Meneja Arsene Wenger, inakutana na Chelsea, ikiwa
chini ya Jose Mourinho, hii ikiwa Himaya ya Pili yake, haijafungwa hata
Mechi moja na Arsenal ya Wenger.
Uso kwa Uso, Arsenal ya Wenger imekutana na Chelsea ya Mourinho mara 9 katika Miaka 9 na Kufungwa mara 5 na Sare 4.
Arsenal v Chelsea
Hali za Wachezaji:
Sentahafu wa Arsenal Laurent Koscielny hatacheza baada ya kuchanika Gotini walipofungwa na Man City Wiki iliyopita.
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ndio
anaanza Kifungo cha Mechi mbili na hivyo hatacheza lakini Lukas Podolski
yuko fiti na anaweza kucheza.
Chelsea wanaweza kuwa nae Beki wao
Branislav Ivanovic ambae anatoka Kifungoni na hii inamaanisha Cesar
Azpilicueta atarudi Fulbeki ya kushoto na Ashley Cole kwenda Benchi.
Chelsea itamkosa Michael Essien ambae anatumikia Kifungo cha Mechi 1 baada kukusanya Kadi za Njano 5.
Tathmini
Wengi hawakuwa wakiipa nafasi kubwa Arsenal kukaa kileleni mwa Ligi kwa muda mrefu nabaada
kuingia Kipindi kigumu kilichoanza kwa Sare na Everton kisha kufungwa
na Napoli kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na kubamizwa Bao 6-3 na Man City
katika Mechi yao ya Ligi iliyopita, Wadau hao wanaichukulia Mechi hii na
Chelsea kama kielelezo cha imani yao.
Mechi hii inachukuliwa kama ndio itaamua
kama Arsenal wanaweza kumudu mbio ndefu za Ubingwa maana ushindi
utawarudisha tena kileleni mwa Ligi.
Lakini Chelsea nao wana matatizo yao
,maana Jumatano iliyopita walifungwa na kutupwa nje ya Capital One Cup
na Sunderland ambayo kwenye Ligi ipo mkiani.
Pia, Meneja wao, Jose Mourinho, amekiri
Timu yake ina matatizo makubwa ya ufungaji Magoli kwa kumkosa kile
alichokiita ‘Straika Muuaji.’
Lakini pia, Msimu huu Chelsea
wameshawahi kushinda Uwanjani Emirates walipoichapa
Arsenal Bao 2-0
kwenye Mechi ya Raundi iliyopita ya Capital One Cup.

Ikiwa Arsenal watafungwa, hii itakuwa ni
mara ya kwanza kufungwa Mechi 3 mfululizo tangu Mwaka 2010 walipofungwa
mara 3 mfululizo na Barcelona, Tottenham na Wigan.
Uso kwa Uso
-Chelsea wameshinda Mechi 3 zilizopita dhidi ya Arsenal mara ya mwisho ikiwa Oktoba 29 Bao 2-0.
-Arsene Wenger hajawahi kumfunga Jose Mourinho katika Mechi 9 akipata Sare 4 na Kufungwa 5.