Lakini, Mchezaji huyo aliezichezea
Liverpool na pia Manchester United ambayo alifanikiwa nayo kutwaa
Ubingwa, amekiri kuwa Liverpool ni tofauti kwani wanao uwezo wa kutwaa
Ubingwa ingawa anaamini Manchester City ndio wenye nafasi kubwa.
Ili Arsenal kutwaa Ubingwa, Michael Owen
anaamini Nyota wao waliemsaini kwa Dau la Rekodi ya Klabu la Pauni
Milioni 42 kutoka Real Madrid, Mesut Ozil, anapaswa kung’ara kila Mechi
badala ya kuonyesha cheche Mechi moja na kisha kufifia Mechi nyingine
tano.
Hadi sasa Ozil ameifungia Arsenal Bao 4
tangu atue hapo Mwezi Agosti na kusaidia kufunga Bao kadhaa lakini,
Michael Owen, akiandika Ripoti yake ya Nusu Msimu kwenye Mtandao wa
Sportlobster, ameeleza: “Licha ya kubamizwa hivi karibuni, Arsenal
wanastahili kuongoza Ligi lakini Timu hiyo inakosa Wachezaji wenye
kiwango cha kwenda mguu kwa mguu na Wapinzani wengine wanaowania
Ubingwa. Licha ya Watu kuniambia mie kuwa Mesut Ozil ana kiwango cha
Dunia, Mchezaji huyo hana uchezaji wa kiwango cha juu cha kudumu kila
Mechi kwani tunamuona mara chache aking’ara na hufuata Mechi kadhaa
akiwa amefifia!”
Owen hana wasiwasi mkubwa na Liverpool
ambao amewaelezea: “Liverpool wanastahili sana kuaambiwa ni moja ya Timu
inayopigania Ubingwa. Sasa wamerudi kwenye Klabu kubwa za juu. Nasikia
Liverpool wanazo Fedha za kuingia Sokoni na kununua Wachezaji Dirisha la
Uhamisho likifunguliwa. Ikiwa Brendan Rodgers atafanikiwa kupata lulu,
siwezi kupinga wao kutwaa Taji ifikapo Mei.”HUU NDIO MSIMAMO WA LIGU KUU ENGLAND MPAKA SASA
| TIMU |
P |
GD |
PTS |
|
1 Arsenal |
16 |
16 |
35 |
|
2 Liverpool |
16 |
21 |
33 |
|
3 Chelsea |
16 |
14 |
33 |
|
4 Man City |
16 |
29 |
32 |
|
5 Everton |
16 |
12 |
31 |
|
6 Newcastle |
16 |
-1 |
27 |
|
7 Tottenham |
16 |
-6 |
27 |
|
8 Man United |
16 |
6 |
25 |
|
9 Southampton |
16 |
5 |
24 |
|
10 Swansea |
16 |
1 |
20 |
|
11 Aston Villa |
16 |
-5 |
19 |
|
12 Hull |
16 |
-6 |
19 |
|
13 Stoke |
16 |
-5 |
18 |
|
14 Norwich |
16 |
-14 |
18 |
|
15 Cardiff |
16 |
-10 |
17 |
|
16 West Brom |
16 |
-5 |
15 |
|
17 West Ham |
16 |
-6 |
14 |
|
18 Crystal Palace |
16 |
-13 |
13 |
|
19 Fulham |
16 |
-15 |
13 |
|
20 Sunderland |
16 |
-18 |
9 |