![]() |
Carvalho amekuwa akitazamwa na United katika matukio kadhaa msimu huu |
Manchester
United wanafikiria kudaka saini ya kiungo wa Sporting Lisbon William
Carvalho katika jaribio la muendelezo wa mpango wao wa kusaka mchezaji
wa kuziba pengo.
United
imekua ikisaka kiungo mkabaji katika viwanja mbalimbali ikiwa ni pamoja
na kumfuatialia katika mchezo uliomalizika kwa suluhu ya 0-0 baina ya
Sporting dhidi ya Porto Jumapili, hii ikiwa ni kwa mujibu wa A Bola.
Taarifa
nchini Ureno zinaarifu kuwa United imekuwa ikimfuatialia mchezaji huyo
katika michezo saba tofauti katika nusu ya kwanza ya kampeni ya ligi ya
Ureno wakati huu ambapo David
Moyes anasaka nyongeza katika kuongeza uwezo wa kikosi chake katika
sehemu ya kiungo.

Carvalho
huenda akavunjiwa mkataba wake kwa karibu pauni milioni £37 ingawa
United itataka mchezaji wa bei ya chini zaidi ya hiyo.
Carvalho
mwenye umri wa miaka 21, alianza kwa mara ya kwanza kuichezea Ureno
kimataifa katika michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya
Sweden mwezi Novemba na anatazamiwa kupata nafasi katika kikosi cha
Paulo Bento katika michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Mkataba
wake unatarajiwa kumalizika 2018 na anaelewa juu ya uwezekano wa
kuvunjwa kwa mkataba wake kwa pauni milioni £37 ingawa United ina
matumaini ya kufanya mazungumzo ya kupunguziwa bei ya mchezaji huyo.
Inaamika kuwa meneja wa United angependa kuongeza wachezaji wawili wa kiungo.