ADNAN JANUZAJ ATEULIWA KUWANIA TUZO KIJANA BORA MICHEZONI!!
CHIPUKIZI
kutoka Manchester United, Adnan Januzaj, amewekwa kwenye Listi ya
Wagombea wa Tuzo ya BBC Young Sports Personality of the Year, ambayo
hutunukiwa Kijana Bora Michezoni kwa kila Mwaka.
Waandaaji wa Tuzo hiyo ni BBC, Shirika la Utangazaji la BBC.
Januzaj, mwenye Miaka 18 na ambae Msimu
huu ameanza kuichezea Timu ya Kwanza ya Mabingwa wa England, Man United,
anasakwa kuzichezea Timu za Taifa za Belgium, Albania, Turkey na
Serbia, ambazo ana uhalali wa kuzichezea lakini pia ataweza kuichezea
England akifikisha Miaka 5 ya kuishi Nchini humo.
Listi hiyo ya Wagombea wa Tuzo ya BBC
Young Sports Personality of the Year inayo Vijana 10 toka Michezo
mbalimbali na itapunguzwa na kubakisha Wanamichezo watatu hapo Desemba
12 na Mshindi kutangazwa Desemba 15.
LISTI WAGOMBEA WA TUZO YA BBC YOUNG SPORTS PERSONALITY OF THE YEAR:
Dina Asher-Smith – Riadha
James Guy – Kuogelea
Amber Hill – Kulenga Shabaha
Charley Hull – Gofu
Adnan Januzaj – Football
Jessica Judd – Riadha
Amy Marren – Paralympic Kuogelea [Walemavu]
Rebekah Tiler – Kunyayua Vyuma
Isaac Towers – Riadha [Wheelchair]
Kimberley Woods – Mashua [Slalom]