Atletico Madrid bado wanamlilia Diego Costa ambaye ana kiu ya kuchezea Ligi ya England
![]() |
| Mkurugenzi wa masuala ya soka wa Atletico Madrid Jose Luis Caminero ana matumaini kuwa Diego Costa (pichani kushoto) hana nia ya kuondoka mwezi Januari |
Mkurugenzi
wa maasula ya soka wa Atletico Madrid
Jose Luis Caminero ana matumaini kuwa mshambuliaji Diego Costa hana nia
ya kuelekea katika ligi ya kuu ya England (Premier League) mwezi
januari.
Costa
amefunga jumla ya mabao 19 katika jumla ya michezo 17 ya Primera
Division mpaka sasa msimu huu na amekuwa akihushwa na usajili ya pesa
nyingi kuelekea katika vilabu viwili vya Arsenal na Chelsea.
Lakini
Caminero anaamini mshambuliaji huyo Mbrazil ambaye amejidhatiti
kuichezea Hispania kimataifa hapo baadaye atasalia Madrid.
Mshambuliaji Costa ana magoli 23 katika jumla ya michezo 21 msimu huu anatakiwa na vilabu vya Arsenal na Chelsea
Akikaririwa na gazeti la Marca amkurugenzi huyo amesema 'Kwasasa Costa hafikirii kuondoka amejidhatiti na Atletico.
'ameongeza mkataba na sisi jambo ambalo ni muhimu. Ameonyesha kuendelea na klabu hii.'
Katika hatua nyingine imeelezwa kuwa endapo Costa ataamua kuondoka Rojiblanco,
Atletico inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa Christian
Benteke.
Mbadala: Kama Costa ataondoka, Atletico inasema itamsaka Christian Benteke(pichani juu) kuziba nafasi yake
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 raia wa Belgium amekuwa akionekana kama mwenye kiwango tangu msimu uliopita.
Kujitokeza
kwa maumivu kwa upande wake kumekuwa ni sababu ya mshambuliaji huyo
kuwepo au kutokuwepo katika kikosi cha klabu hiyo huku tayari amesha
tupia wavuni magoli matano msimu huu goli la mwisho akifunga Septemba
14.
Costa amethaminishwa kwa pauni milioni £32 za kuvunja mkataba wake lakini Arsenal
inaonekana kutokuwa tayari kufikia kiwango hicho ili kupata huduma yake.www.fulu viwanja blogspot.com
