Arsenal yajiimarisha kwa mabao

Arsena iko mbele ya Chelsea kwa pointi nne
Bao la kwanza la mchezaji
Nicklas Bendtner tangu Machi mwaka 2011, lilisaidia Arsenal kuicharaza
Hull na kujiweka katika nafasi nzuri mbele ya washindani wao kwenye ligi
ya Premier.
Bao la Bendtner lilitokana na mkwaju wa Carl
Jenkinson huku Bendtner akisema kuwa limekuwa jambo gumu sana kwake
kuona Arsenal wakipanda ngazi wakati wote akiwa mchezaji wa akiba.
Bao lengine liliingizwa na Mesut
Ozil, kutokana na mkwaju wa Aaron Ramsey, na kufikisha mabao yao kuwa
mawili kwa nunge katika dakika ya 47.
Mchezaji wa Hull, Jake Livermore nusura aingize bao lao la kwanza ingawa mlinda lango Wojciech Szczesny alilinyakua.
Meneja wa Hull, Steve Bruce, alisema kua
halikuwa jambo la busara kuchezesha, washambululiaji wawili ili kutafuta
pointi baada ya kupata ushindi wa ghafla dhidi ya Liverpool.
Arsenal sasa wana pointi nne mbele ya Chelsea
huku wakiendelea kujizatiti katika kinyang'anyiro hiki cha kombe la Ligi
ya Premier.