Timu zote hizo zimecheza Mechi 11 kila mmoja.
Huko Mjini Mbeya, ambako Timu za Mji huo zilipambana, Mbeya City iliichapa Tanzania Prisons Bao 2-0.
Jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Mabingwa Yanga waliibamiza Mgambo Shooting Bao 3-0.
Hadi Mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 31 la Mbuyu Twite.
Kipindi cha Pili, katika Dakika ya 50,
Hamis Kiiza alifunga Bao la pili kwa Penati kufuatia Kipa wa Mgambo
kumchezea faulo Didier Kavumbagu.
Bao la Tatu lilifungwa Dakika ya 67 na Didier Kavumbagu.