Simba walifunga Bao la katika Dakika ya
23 kwa Bao la Ramadhan Singano ‘Messi’ lakini Kipre Tchetche
akaisawazshia Azam FC katika Dakika ya 43.
Katika Dakika ya 72, Kipre Tchetche tena
alikwamisha Mpira wavuni na kuipa ushindi Azam FC na kuwafanya wakae
kileleni wakiwa na Pointi 23 kwa Mechi 11 wakifuata Simba ambao pia
wamecheza Mechi 11 na wamebaki na Pointi 20.
Huko Mkwakwani, Tanga, Wenyeji Coastal
Union wameichapa Mtibwa Sugara Bao 3-0 na Bao zao kufungwa na Crispian
Odula, Jerry Santo na Danny Lyanga.
Kesho Jumanne, Mabingwa Watetezi Yanga
watajimwaga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuivaa Timu ya mkiani Mgambo
Shooting na ushindi kwa Yanga utawafanya wawazidi Simba kwa Pointi.LIGI HIYO ITAENDELE KESHO KWA VIWANJA VITATU KUWAKA MOTO;
Tanzania Prisons vs Mbeya City
Yanga vs Mgambo Shooting
Rhino Rangers vs JKT Ruvu